MEI: ULIMWENGU WA FEDHA
Uchumi wa kweli, ambao unatengeneza ajira, upo katika kipeo cha mgogoro. Ni watu wangapi ambao hawana ajira!- Lakini masoko ya fedha hayajawahi kuongezeka kama yalivyo sasa hivi. Ulimwengu wa juu wa fedha upo umbali gani kutoka kwenye maisha ya watu wa kawaida! Kama fedha haitadhibitiwa, itakuwa ni dhahania zinazoendeshwa na sera mbalimbali za kifedha. Hali hii si endelevu. Na ni hatari. Ili masikini wasisumbuke na madhara ya maumivu ya mfumo huu, dhahania ya kifedha ni lazima idhibitiwe kwa uangalifu. Dhahania. Nataka kulitia mkazo neno hilo. Fedha iwe aina ya mfumo wa huduma na chombo cha kuwahudumia watu na kuwatunza katika makao ya pamoja. Bado tuna muda wa kuanza mchakato huu wa mbadiliko ya dunia! Kuifanyia kazi aina nyingine ya uchumi, ambao ni wa haki, wa pamoja na wa kudumu. Tunaweza kulifanya hili! Na tuombe ili wale walio na dhima ya fedha washirikiane na serikali kudhibiti eneo la fedha na kuwalinda wananchi dhidi ya hatari zake.